عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بنِ مسعُودٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ:
ذُكِرَ عِنْدَ النَّبِيِّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ رَجُلٌ نَامَ لَيْلَهُ حَتَّى أَصْبَحَ، قَالَ: «ذَاكَ رَجُلٌ بَالَ الشَّيْطَانُ فِي أُذُنَيْهِ، أَوْ قَالَ: فِي أُذُنِهِ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 3270]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abdullahi bin Masoud -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema:
Alitajwa kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake mtu mmoja aliyelala usiku mpaka pakapambazuka, akasema: "Huyo ni mtu aliyekojolewa na Shetani ndani ya masikio yake, au alisema: ndani ya sikio lake".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 3270]
Alitajwa kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake mtu mmoja aliyelala mpaka pakapambazuka na Jua likachomoza na wala hakunyanyuka kwenda katika swala ya faradhi, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Huyo ni mtu ambaye Shetani kakojoa ndani ya sikio lake.