عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الخُدْرِيِّ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«إِذَا سَمِعْتُمُ النِّدَاءَ، فَقُولُوا مِثْلَ مَا يَقُولُ المُؤَذِّنُ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 611]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Saidi Al-Khudry -Radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-:
"Mtakaposikia wito (Adhana), basi semeni mfano wa yale ayasemayo muadhini".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 611]
Anahimiza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kumjibu muadhini wakati wa kumsikia, na hii ni kwa sisi kusema mfano wa ayasemayo, sentensi kwa sentensi, Anaposema Allaahu Akbaru nasi tunasema Allaahu Akbaru, na anapotamka shahada mbili, nasi tunazitamka baada yake, Linaondolewa tamko la: (Hayya a'las swalaa, Hayya a'lal falaah) hapo tutasema baada yake: Laa haulaa walaa quwwata illaa billaah.