«مَنْ قَرَأَ حَرْفًا مِنْ كِتَابِ اللهِ فَلَهُ بِهِ حَسَنَةٌ، وَالْحَسَنَةُ بِعَشْرِ أَمْثَالِهَا، لَا أَقُولُ {الم} حَرْفٌ، وَلَكِنْ {أَلِفٌ} حَرْفٌ، وَ{لَامٌ} حَرْفٌ، وَ{مِيمٌ} حَرْفٌ».
[حسن] - [رواه الترمذي] - [سنن الترمذي: 2910]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abdallah bin Masoud -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- akisema:
"Atakayesoma herufi moja katika kitabu cha Allah basi atapata jema moja kwa herufi hiyo, na jema hilo hulipwa mara kumi mfano wake, sisemi (Alif Laam Miim) ni herufi, lakini (Alif) ni herufi, na (Laam) ni herufi, na (Miim) ni herufi".
Ameeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa kila muislamu anayesoma herufi moja katika kitabu cha Mwenyezi Mungu basi atapata jema moja kwa herufi hiyo, na huzidishiwa malipo hayo mpaka mara kumi mfano wake.
Kisha akaliweka wazi hilo kwa kauli yake: (Sisemi "Alif Laam Miim" ni herufi, lakini Alif ni herufi, na Laam ni herufi, na Miim ni herufi): Inakuwa herufi zote tatu zina thawabu thelathini (30).
الحث على الإكثار من تلاوة القرآن.على قرون الموج في