عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«كُلُّ سُلاَمَى مِنَ النَّاسِ عَلَيْهِ صَدَقَةٌ، كُلَّ يَوْمٍ تَطْلُعُ فِيهِ الشَّمْسُ يَعْدِلُ بَيْنَ الِاثْنَيْنِ صَدَقَةٌ، وَيُعِينُ الرَّجُلَ عَلَى دَابَّتِهِ فَيَحْمِلُ عَلَيْهَا أَوْ يَرْفَعُ عَلَيْهَا مَتَاعَهُ صَدَقَةٌ، وَالكَلِمَةُ الطَّيِّبَةُ صَدَقَةٌ، وَكُلُّ خُطْوَةٍ يَخْطُوهَا إِلَى الصَّلاَةِ صَدَقَةٌ، وَيُمِيطُ الأَذَى عَنِ الطَّرِيقِ صَدَقَةٌ».

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:
"Kila kiungo kwa watu kina sadaka, kila siku inayochomozewa jua: Ukafanya uadilifu kati ya watu wawili ni sadaka, na ukimsaidia mtu katika mnyama wake ukambeba kumpandisha au ukamnyanyulia mzigo wake ni sadaka, na neno zuri ni sadaka, na kwa kila hatua unayokwenda kuelekea msikitini ni sadaka, na ukiondoa maudhi njiani ni sadaka".

Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake Swahiih Al Bukhaariy - 2989

Ufafanuzi

Mtume rehema na amani ziwe juu yake ameeleza kuwa kila Muislamu ni wajibu kila siku kuhesabu kila kiungo cha mifupa yake kuwa ni sadaka ya hiyari kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na kuwa ni njia ya kumshukuru kwa neema ya afya, na kwamba amevifanya viungo vyake kuwa na maungio yanayomuwezesha kukunja na kukunjua, Sadaka hii inafanywa na matendo yote mema na haitegemei kutoa pesa, na miongoni mwake: Uadilifu wako na kusuluhisha kwako kati ya wagomvi wawili ni sadaka, Na katika kumsaidia kwako asiyejiweza kupanda katika mnyama wake, ukambeba, au ukamnyanyulia mzigo, ni sadaka. na neno zuri kuanzia kumtaja Mwenyezi Mungu na dua na salamu na mengineyo, ni sadaka, na kwa kila hatua unayoipiga kwenda katika swala, ni sadaka, na kuondoa kila yanayoudhi katika njia ni sadaka.

Katika Faida za Hadithi

  1. Muundo wa mifupa na viungo vya mwanadamu ni moja ya neema kubwa za Mwenyezi Mungu juu yake, hivyo kila mfupa peke yake unahitaji kutolewa sadaka kwa niaba yake ili itimie kushukuru neema hiyo.
  2. Himizo la kurudia upya shukurani kila siku ili neema hizo zidumu.
  3. Himizo la kudumu kufanya ibada za sunna na sadaka kila siku.
  4. Fadhila ya kusuluhisha baina ya watu.
  5. Himizo la mtu kumsaidia ndugu yake; kwani msaada wake kwake ni sadaka.
  6. Himizo la kuhudhuria swala za pamoja na kuziendea, na kuimarisha misikiti kwa hilo.
  7. Uwajibu wa kuheshimu njia wanazopita waumini kwa kuepuka yanayo waudhi au kuwadhuru.

Kuonyesha Tafsiri

62 Lugha
EN English الإنجليزية
UR اردو الأوردية
ES Español الإسبانية
ID Indonesia الإندونيسية
UG ئۇيغۇرچە الأيغورية
BN বাংলা البنغالية
FR Français الفرنسية
TR Türkçe التركية
RU Русский الروسية
BS Bosanski البوسنية
SI සිංහල السنهالية
HI हिन्दी الهندية
ZH 中文 الصينية
FA فارسی الفارسية
VI Tiếng Việt الفيتنامية
TL Tagalog تجالوج
KU Kurdî الكردية
HA Hausa الهوسا
PT Português البرتغالية
ML മലയാളം المليالم
TE తెలుగు التلغو
TA தமிழ் التاميلية
TH ไทย التايلندية
DE Deutsch الألمانية
JA 日本語 اليابانية
PS پښتو بشتو
AS অসমীয়া الأسامية
SQ Shqip الألبانية
SV Svenska السويدية
AM አማርኛ الأمهرية
NL Nederlands الهولندية
GU ગુજરાતી الغوجاراتية
KY Кыргызча القيرقيزية
NE नेपाली النيبالية
YO Yorùbá اليوروبا
LT Lietuvių الليتوانية
PRS دری الدرية
SR Српски الصربية
SO Soomaali الصومالية
TG тоҷикӣ الطاجيكية
RW Kinyarwanda الكينياروندا
RO Română الرومانية
HU Magyar المجرية
CS Čeština التشيكية
MOS Moore الموري
MG Malagasy المالاجاشية
OM Oromoo الأورومو
KN ಕನ್ನಡ الكانادا
WO Wolof الولوف
AZ Azərbaycan الأذربيجانية
UZ O‘zbek الأوزبكية
UK Українська الأوكرانية
KA ქართული الجورجية
MK Македонски المقدونية
KM ភាសាខ្មែរ الخميرية
BM Bambara البامبارية
PA ਪੰਜਾਬੀ البنجابية
MR मराठी الماراثية
DA Dansk الدنماركية
RN Kirundi الكيروندي
KMR Kurmancî الكرمنجية
MS Bahasa Melayu الملايو