1. Nyumbani
  2. Aina tofauti tofauti
  3. Fiq'hi na misingi yake.

Hadithi Atakayefunga siku moja katika njia ya Mwenyezi Mungu, atauweka mbali Mwenyezi Mungu uso wake na moto miaka sabini

عَنْ أَبِي سَعِيدٍ الْخُدْرِيِّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ:
«مَنْ صَامَ يَوْمًا فِي سَبِيلِ اللهِ بَاعَدَ اللهُ وَجْهَهُ عَنِ النَّارِ سَبْعِينَ خَرِيفًا».

Imepokelewa na Abii Said Al-khuduriy -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake- akisema:
"Atakayefunga siku moja katika njia ya Mwenyezi Mungu, atauweka mbali Mwenyezi Mungu uso wake na moto miaka sabini".

Sahihi Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake Swahiih Muslim - 1153

Ufafanuzi

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayefunga siku moja katika Jihadi na kwingineko kwa kutakasa nia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, kwa kutafuta thawabu na malipo kutoka kwa Mwenyezi Mungu; basi Mwenyezi Mungu kwa fadhila zake ataweka mbali baina yake na moto miaka sabini.

Katika Faida za Hadithi

  1. Amesema Nawawi: Fadhila za kufunga katika njia ya Mwenyezi Mungu, na hili linachukuliwa kwa yule ambaye hadhuriki kwa swaumu hiyo, na wala hapotezi haki zake, na wala hatopoteza mapambano yake wala kinginecho katika majukumu mapigano yake.
  2. Himizo na hamasisho la kufunga swaumu ya hiyari.
  3. Uwajibu wa kutakasa nia kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na wala asifunge kwa kujionyesha wala kutaka kusikika, wala kwa makusudio mengine.
  4. Amesema As-sanadi: Kauli yake "Katika njia ya Mwenyezi Mungu", inategemea kuwa masukudio yake ni nia pekee, na inawezekana kuwa makusudio yake nikuwa amefunga akiwa katika hali ya vitani, na la pili ndio liko karibu na usawa.
  5. Amesema bin Hajari: Kauli yake: "Viangazi sabini" Kiangazi ni wakati maalumu wa mwaka, na makusudio yake hapa ni mwaka, na kutajwa kiangazi pekee hapa pasina kutaja wakati uliobakia -kama kiangazi na masika, na kipupwe-; kwa sababu kiangazi ndio kipindi kizuri zaidi kwani hua ndio muda wa kuvuna matunda.

Kuonyesha Tafsiri

47 Lugha
EN English الإنجليزية
UR اردو الأوردية
ES Español الإسبانية
ID Indonesia الإندونيسية
UG ئۇيغۇرچە الأيغورية
BN বাংলা البنغالية
TR Türkçe التركية
RU Русский الروسية
BS Bosanski البوسنية
SI සිංහල السنهالية
HI हिन्दी الهندية
ZH 中文 الصينية
FA فارسی الفارسية
VI Tiếng Việt الفيتنامية
TL Tagalog تجالوج
KU Kurdî الكردية
HA Hausa الهوسا
PT Português البرتغالية
ML മലയാളം المليالم
TE తెలుగు التلغو
TA தமிழ் التاميلية
MY မြန်မာ البورمية
TH ไทย التايلندية
DE Deutsch الألمانية
PS پښتو بشتو
AS অসমীয়া الأسامية
SQ Shqip الألبانية
SV Svenska السويدية
AM አማርኛ الأمهرية
NL Nederlands الهولندية
GU ગુજરાતી الغوجاراتية
NE नेपाली النيبالية
PRS دری الدرية
SR Српски الصربية
RO Română الرومانية
HU Magyar المجرية
MOS Moore الموري
MG Malagasy المالاجاشية
OM Oromoo الأورومو
KN ಕನ್ನಡ الكانادا
WO Wolof الولوف
UK Українська الأوكرانية
KA ქართული الجورجية
MK Македонски المقدونية
KM ភាសាខ្មែរ الخميرية
PA ਪੰਜਾਬੀ البنجابية
MR मराठी الماراثية