عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضيَ اللهُ عنهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«إِذَا انْتَهَى أَحَدُكُمْ إِلَى الْمَجْلِسِ فَلْيُسَلِّمْ، فَإِذَا أَرَادَ أَنْ يَقُومَ فَلْيُسَلِّمْ، فَلَيْسَتِ الْأُولَى بِأَحَقَّ مِنَ الْآخِرَةِ».
[حسن] - [رواه أبو داود والترمذي والنسائي في الكبرى وأحمد] - [سنن أبي داود: 5208]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume -rehema na amani ziwe juu yake-:
"Atakapofika mmoja wenu katika kikao basi na atoe salamu, na akitaka kunyanyuka pia atoe salamu, kwani ya mwanzo haina haki zaidi kuliko ya mwisho".
[Ni nzuri] - [Imepokelewa na An-Nasaaiy] - [سنن أبي داود - 5208]
Alimuelekeza Mtume rehema na amani ziwe juu yake atakayekuja mahali walipokaa watu basi awasalimie, na akitaka kunyanyuka basi awaage jamaa zake pia kwa salamu; kwani salamu ya kwanza wakati wa kuja si bora sana kuliko salamu ya mwisho wakati wa kuondoka.