عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضيَ اللهُ عنهُ:
أَنَّ رَجُلًا دَخَلَ المَسْجِدَ يَوْمَ جُمُعَةٍ مِنْ بَابٍ كَانَ نَحْوَ دَارِ القَضَاءِ، وَرَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَائِمٌ يَخْطُبُ، فَاسْتَقْبَلَ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَائِمًا، ثُمَّ قَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، هَلَكَتِ الأَمْوَالُ وَانْقَطَعْتِ السُّبُلُ، فَادْعُ اللَّهَ يُغِيثُنَا، فَرَفَعَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَدَيْهِ، ثُمَّ قَالَ: «اللَّهُمَّ أَغِثْنَا، اللَّهُمَّ أَغِثْنَا، اللَّهُمَّ أَغِثْنَا» قَالَ أَنَسٌ: وَلا وَاللَّهِ، مَا نَرَى فِي السَّمَاءِ مِنْ سَحَابٍ وَلَا قَزَعَةً، وَمَا بَيْنَنَا وَبَيْنَ سَلْعٍ مِنْ بَيْتٍ وَلَا دَارٍ، قَالَ: فَطَلَعَتْ مِنْ وَرَائِهِ سَحَابَةٌ مِثْلُ التُّرْسِ، فَلَمَّا تَوَسَّطَتِ السَّمَاءَ انْتَشَرَتْ، ثُمَّ أَمْطَرَتْ، فَلَا وَاللَّهِ، مَا رَأَيْنَا الشَّمْسَ سِتًّا، ثُمَّ دَخَلَ رَجُلٌ مِنْ ذَلِكَ البَابِ فِي الجُمُعَةِ، وَرَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَائِمٌ يَخْطُبُ، فَاسْتَقْبَلَهُ قَائِمًا، فَقَالَ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، هَلَكَتِ الأَمْوَالُ، وَانْقَطَعَتِ السُّبُلُ، فَادْعُ اللَّهَ يُمْسِكْهَا عَنَّا، قَالَ: فَرَفَعَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَدَيْهِ، ثُمَّ قَالَ: «اللَّهُمَّ حَوَالَيْنَا وَلَا عَلَيْنَا، اللَّهُمَّ عَلَى الآكَامِ وَالظِّرَابِ، وَبُطُونِ الأَوْدِيَةِ، وَمَنَابِتِ الشَّجَرِ» قَالَ: فَأَقْلَعَتْ، وَخَرَجْنَا نَمْشِي فِي الشَّمْسِ، قَالَ شَرِيكٌ: سَأَلْتُ أَنَسَ بْنَ مَالِكٍ: أَهُوَ الرَّجُلُ الأَوَّلُ؟ فَقَالَ: «مَا أَدْرِي».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 1014]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Anas bin Maalik -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-:
Ya kwamba mtu mmoja aliingia msikitini siku ya Ijumaa kupitia mlango uliokuwa upande wa Dar Al-Kadhaa, na huku Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesimama akihutubu, akamuelekea Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa wima, kisha akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, mali zimeteketea na njia zote zimekatika, muombe Mwenyezi Mungu atuletee mvua, akanyanyua Mtume rehema na amani ziwe juu yake mikono yake, kisha akasema: "Ewe Mola wetu tunyeshelezee, Ewe Mola wetu tunyeshelezee, Ewe Mola wetu tunyeshelezee". Akasema Anasi: Namuapa Mwenyezi Mungu, hatukua tukiona mbinguni mawingu wala dalili, na kati yetu na Mlima Sal'i hapakuwa na nyumba wala makazi, anasema: Likachomoza wingu nyuma yake mithili ya ngao, lilipofika kati kati ya mawingu likatanda kote, kisha mvua ikaanza kunyesha, namuapa Mwenyezi Mungu hutukuliona Jua kwa muda wa siku , kisha akaingia bwana mmoja kupitia mlango ule ule siku ya Ijumaa na Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa wima akihutubia, akamuelekea akiwa kasimama akasema ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, mali zimeangamia, na njia zimekatika, muombe Mwenyezi Mungu aizuie kwetu mvua, anasema akanyanyua Mtume rehema na amani ziwe juu yake mikono yake, kisha akasema: "Ewe Mwenyezi Mungu inyeshe pembezoni mwetu na si juu yetu, ewe Mwenyezi Mungu inyeshe katika vichuguu na milima na ndani ya mabonde, na katika maoteo ya miti" Anasema: Mvua ikakata, na tukatoka tukitembea juani, amesema Shariki: Nilimuuliza Anasi, je ni yule yule mtu wa kwanza? Akasema: "Sijui".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 1014]
Aliingia bedui mmoja msikiti wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake siku ya Ijumaa kupitia mlango wa Magharibi upande wa nyumba ya Omari bin Khattwab radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, na Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa kasimama anahutubia, yule bwana akamuelekea Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na akasema, ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, wanyama wameangamia, na njia zote zimekatika kwa kufa mifugo inayobeba watu, au imedhoofika kutokana na njaa, basi muombe Mwenyezi Mungu atunyeshelezee mvua. Akanyanyua rehema na amani ziwe juu yake mikono yake, kisha akasema: Ewe Mwenyezi Mungu tunyeshelezee, Ewe Mwenyezi Mungu tunyeshelezee, Ewe Mwenyezi Mungu tunyeshelezee. Amesema Anasi bin Maliki radhi za Allah ziwe juu yake: Wallahi hatukua tukiona mbinguni hata kipande cha mawingu, na hapakuwa kati yetu sisi msikitini na Mlima Sal'i ulioko Magharibi mwa msikiti upande ambao hujia mawingu nyumba wala makazi yanayoweza kutuzuia kuona mawingu. Amesema Anasi radhi za Allah ziwe juu yake: Likatokeza nyuma yake wingu la duara mfano wa ngao nayo ni mviringo mdogo, lilipofika kati kati ya mawingu ya Madina likatanda, kisha mvua ikaanza kunyesha, na namuapa Mwenyezi Mungu, hatukuliona Jua tena kutokana na mvua mpaka Ijumaa iliyofuata, kiasi kwamba aliingia tena yule bwana kupitia mlango ule ule, huku rehema na amani ziwe juu yake akiwa kasimama anahutubia, akamuelekea akiwa wima, akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, mali zimeangamia na njia zimekatika, basi muombe Mwenyezi Mungu aizuie mvua kwetu. Akasema: Akanyanyua rehema na amani ziwe juu yake mikono yake, kisha akasema: Ewe Mwenyezi Mungu igeuze mvua iende pembezoni mwetu ewe Mwenyezi Mungu ielekee katika sehemu zenye miinuko katika Ardhi kama kichuguu, na milima midogo, na ndani ya mabonde, na maoteo ya miti. Akasema Anasi: Yakakatika mawingu ya mvua, na tukatoka tukitembea juani.