Aina:
+ -

عَنْ أُمِّ المُؤْمِنِينَ أُمِّ عَبْدِ اللَّهِ عَائِشَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا، قَالَتْ: قَالَ: رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم:
«مَنْ أَحْدَثَ فِي أَمْرِنَا هَذَا مَا لَيْسَ مِنْهُ فَهُوَ رَدٌّ». وَفِي رِوَايَةٍ لِمُسْلِمٍ: «مَنْ عَمِلَ عَمَلًا لَيْسَ عَلَيْهِ أَمْرُنَا فَهُوَ رَدٌّ».

[صحيح] - [رواه البخاري ومسلم] - [الأربعون النووية: 5]
المزيــد ...

Kutoka kwa mama wa waumini mama Abdillah Aisha radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake:
"Yeyote atakayezua (kitu) katika jambo letu hili (dini) ambalo si miongoni mwake, basi hilo litakataliwa."

[Sahihi] - [رواه البخاري ومسلم] - [الأربعون النووية - 5]

Ufafanuzi

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayetunga au kubuni jambo katika dini au akafanya amali yoyote ambayo haikuelekezwa na dalili yoyote kutoka katika Qur'ani na Sunna, basi jambo hilo litarejeshwa kwa mfanyaji wake na halitokubaliwa mbele ya Allah.

Katika Faida za Hadithi

  1. Ibada zote zimejengeka juu ya yale yalikuja katika Qur'ani na Sunna, hatutakiwi kumuabudu Allah Mtukufu isipokuwa kwa sheria aliyoiweka na si kwa uzushi na mambo ya kutungwa.
  2. Dini haiendi kwa rai na kutazama lipi zuri, bali inakwenda kwa kumfuata Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-.
  3. Hadithi hii ni ushahidi wa kukamilika dini.
  4. Uzushi ni kila kilichozushwa katika dini na hakikuwepo katika zama za Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- na Masahaba zake katika itikadi (Aqida) au kauli au amali yoyote.
  5. Hadithi hii ni msingi katika misingi ya Uislamu, nayo ni sawa na mzani kwa matendo, kama ambavyo kila amali ambayo haikukusudiwa kupata radhi za Allah Mtukufu, mfanyaji wake hana thawabu ndani yake, hivyo hivyo kila amali ambayo haitakuwa samabamba na yale aliyokuja nayo Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- basi hiyo itarejeshwa kwa mfanyaji wake.
  6. Hadithi hii ndiyo kanuni katika kukataa uzushi na mambo mageni na maovu yanayotokea.
  7. Uzushi uliokatazwa ni ule unaokuwa katika mambo ya dini na si ya kidunia.
Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Lugha ya Kiindonesia Kibangali Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kimalayo Kitelguu Kunakili kumbukumbu mahala pa kutafsiri Thai German Pashto Kiassam Albanian الأمهرية الغوجاراتية Luqadda qer-qeesiya النيبالية الدرية الصربية الطاجيكية Luqadda kiniya ruwadiga المجرية التشيكية الموري Luqadda kinaadiga الولوف Luqadda Asariga الأوزبكية الأوكرانية الجورجية المقدونية الخميرية
Kuonyesha Tarjama
Aina tofauti
Ziada