عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«مِنْ حُسْنِ إِسْلَامِ المَرْءِ تَرْكُهُ مَا لَا يَعْنِيهِ».
[قال النووي: حديث حسن] - [رواه الترمذي وغيره] - [الأربعون النووية: 12]
المزيــد ...
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake:
"Katika uzuri wa uislamu wa mtu: Ni kuacha kwake yale yasiyomuhusu".
[قال النووي: حديث حسن] - [رواه الترمذي وغيره] - [الأربعون النووية - 12]
Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Ya kuwa miongoni mwa mazuri ya ukamilifu wa Uislamu wa Muislamu na ukamilifu wa imani yake, ni kujiweka kwake mbali na yale yasiyomuhusu na yale yasiyo na faida kwake miongoni mwa kauli na matendo, au katika yale yasiyomuhusu miongoni mwa mambo ya dini na dunia, mtu kushughulika na yale yasiyomuhusu huenda likamshughulisha akaacha yale yanayomuhusu, au likampelekea katika yale yanayomlazimu kuyaepuka; kwani mwanadamu ataulizwa kuhusu matendo yake siku ya Kiyama.