«مَنْ كَذَبَ عَلَيَّ مُتَعَمِّدًا فَلْيَتَبَوَّأْ مَقْعَدَهُ مِنَ النَّارِ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 110]
المزيــد ...
Imepolelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema: Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-:
"Yeyote atakayenisingizia mimi uongo kwa makusudi basi ajiandalie makazi yake kuwa ni motoni".
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayemsemea uongo kwa makusudi kwa kumnasibishia kauli au kitendo kwa uongo, basi atambue kuwa Akhera atakua na makazi motoni; ndio malipo yake kwa kumsingizia kwake uongo.