عن ابن عمر رضي الله عنهما قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم:
«كل مُسْكِرٍ خَمْرٌ، وكل مُسْكِرٍ حرام، ومن شرِب الخمر في الدنيا فمات وهو يُدْمِنُهَا لَمْ يَتُبْ، لَمْ يَشْرَبْهَا في الآخرة».
[صحيح] - [رواه مسلم وأخرج البخاري الجملة الأخيرة منه] - [صحيح مسلم: 2003]
المزيــد ...
kutoka kwa bin Omar -Radhi za Allah ziwe juu yao- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake-
"kila kilevi ni haramu, na atakayekunywa pombe duniani na akafa akiwa mlevi kupindukia na hakutubia, hatoinywa huko akhera"
[Sahihi] - - [صحيح مسلم - 2003]
Amebainisha wazi Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa kila kinachoondosha akili na kuiondoa hicho ni pombe yenye kulewesha, sawa iwe ni kunywa, au kula, au kuvuta kwa pumzi au vinginevyo, na kuwa kila kinacholevya na kuondoa akili Mwenyezi Mungu Mtukufu amekiharamisha na amekataza, kiwe kidogo au kingi, Na kuwa kila mwenye kunywa aina yoyote ya vileo, na akaendelea kuvinywa, wala hakutubia mpaka akafa; Anastahiki adhabu ya Mwenyezi Mungu kwa kumnyima kuinywa Peponi.