«إِنَّ الْعَهْدَ الَّذِي بَيْنَنَا وَبَيْنَهُمُ الصَّلَاةُ، فَمَنْ تَرَكَهَا فَقَدْ كَفَرَ».
[صحيح] - [رواه الترمذي والنسائي وابن ماجه وأحمد] - [سنن النسائي: 463]
المزيــد ...
Kutoka kwa Buraida -Radhi za Allah ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake:
"Hakika ahadi iliyopo kati yetu na wasiokuwa waislamu ni sala, na atakayeiacha sala basi huyo ni kafiri".
Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa ahadi na mkataba kati ya waislamu na wasiokuwa wao katika makafiri na wanafiki ni swala, atakayeiacha atakuwa amekufuru.