+ -

عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضيَ اللهُ عنهُما قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«البَسُوا مِنْ ثِيَابِكُمُ البَيَاضَ، فَإِنَّهَا مِنْ خَيْرِ ثِيَابِكُمْ، وَكَفِّنُوا فِيهَا مَوْتَاكُمْ».

[صحيح] - [رواه أبو داود والترمذي وابن ماجه] - [سنن الترمذي: 994]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa bin Abbas radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake-:
"Vaeni katika nguo zenu nguo nyeupe, kwani hizo ni katika nguo zenu bora, na wavisheni kwazo maiti wenu".

[Sahihi] - - [سنن الترمذي - 994]

Ufafanuzi

Anawaelekeza Mtume rehema na amani ziwe juu yake wanaume kuvaa nguo zenye rangi nyeupe na kuwavisha maiti pia; kwani ni katika nguo bora.

Katika Faida za Hadithi

  1. Sunna ya kuvaa nguo nyeupe, na inafaa pia kuvaa rangi nyingine tofauti na hiyo.
  2. Sunna ya kuwavisha maiti nguo nyeupe.
  3. Amesema Shaukani: Na hadithi inaonyesha sheria ya kuvaa nguo nyeupe na kuwavisha nazo maiti pia; kwakuwa ni safi zaidi na ni nzuri zaidi, ama kuwa kwake ni nzuri hili liko wazi, na ama kuwa kwake ni safi ni kwa sababu kitu chochote hata kikwa kidogo kikidondokea juu yake huonekana, ndio maana inapendekezwa.
Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiindonesia Kisin-hala Kivetenamu Kihausa Thai Kiassam الهولندية الغوجاراتية الرومانية المجرية الجورجية
Kuonyesha Tarjama