عَنْ حُذَيْفَةَ بْنِ اليَمَانِ رَضيَ اللهُ عنه:
أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ إِذَا أَرَادَ أَنْ يَنَامَ وَضَعَ يَدَهُ تَحْتَ رَأْسِهِ، ثُمَّ قَالَ: «اللَّهُمَّ قِنِي عَذَابَكَ يَوْمَ تَجْمَعُ أَوْ تَبْعَثُ عِبَادَكَ».
[صحيح] - [رواه الترمذي] - [سنن الترمذي: 3398]
المزيــد ...
Kutoka kwa Hudheifa bin Yamaani -radhi za Allah ziwe juu yake-:
Ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa anapotaka kulala anaweka mkono wake chini ya kichwa chake, kisha anasema: "Ewe Mwenyezi Mungu nikinge na adhabu yako siku utakapowakusanya au kuwafufua waja wako".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy - Imepokelewa na An-Nasaaiy - Imepokelewa na Abuu Daud - Imepokelewa na Ahmad] - [سنن الترمذي - 3398]
Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapochukua malazi yake kwa ajili ya kulala, anauchegemea mkono wake wa kulia na anauwekea shavu lake la kulia, akasema: "Ewe Mwenyezi Mungu" Mola wangu Mlezi "Nikinge" na unihifadhi kutokana na "adhabu yako" na mateso yako "siku utakapowakusanya au kuwafufua waja wako" katika siku ya hesabu, siku ya Kiyama.