عن أَبِي أُمَامَةَ إِياسِ بنِ ثَعْلَبَةَ الحَارِثِيِّ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ:
«مَنِ اقْتَطَعَ حَقَّ امْرِئٍ مُسْلِمٍ بِيَمِينِهِ، فَقَدْ أَوْجَبَ اللهُ لَهُ النَّارَ، وَحَرَّمَ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ» فَقَالَ لَهُ رَجُلٌ: وَإِنْ كَانَ شَيْئًا يَسِيرًا يَا رَسُولَ اللهِ؟ قَالَ: «وَإِنْ قَضِيبًا مِنْ أَرَاكٍ».
[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 137]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Umama Iyaasi bin Tha'laba Al-Haarithy radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema:
"Atakayejikatia haki ya muislamu kwa mkono wake wa kulia, basi Mwenyezi Mungu atakuwa kamuwajibishia moto, na kamharamishia pepo" Bwana mmoja akamuuliza: Hata kikiwa kitu kidogo ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: "Hata kikiwa kijiti cha mswaki wa Araki".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 137]
Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuapa uongo kwa jina la Mwenyezi Mungu ili kujikatia haki ya muislamu, kwani malipo ya hilo ni kustahiki moto, na kunyimwa pepo, nalo ni katika madhambi makubwa. Bwana mmoja akasema ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu: Hata kikiwa kilichoapiwa ni kitu kidogo? Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Hata kikiwa ni kijiti cha mswaki unaochukuliwa kutoka katika mti wa Araki.