عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«انْصُرْ أَخَاكَ ظَالِمًا أَوْ مَظْلُومًا». فَقَالَ رَجُلٌ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، أَنْصُرُهُ إِذَا كَانَ مَظْلُومًا، أَفَرَأَيْتَ إِذَا كَانَ ظَالِمًا كَيْفَ أَنْصُرُهُ؟ قَالَ: « تَحْجُزُهُ -أَوْ تَمْنَعُهُ- مِنَ الظُّلْمِ؛ فَإِنَّ ذَلِكَ نَصْرُهُ».
[صحيح] - [رواه البخاري] - [صحيح البخاري: 6952]
المزيــد ...
Imepokewa kutoka kwa Anas bin Maliki -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake:
"Msaidie ndugu yako akiwa amedhulumu au kudhulumiwa", Akasema mtu mmoja: Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, unaonaje ikiwa ndugu yangu kadhulumu, vipi nitamsaidia? Akasema: "Unamuhama au unamzuia asifanye dhulma, kwa kufanya hivyo ndiyo kumnusuru".
[Sahihi] - [Imepokelewa na Al-Bukhaariy] - [صحيح البخاري - 6952]
Mtume rehema na amani ziwe juu yake amemuamrisha Muislamu kumsadia ndugu yake Muislamu sawa sawa awe kadhulumu au kadhulumiwa, mtu mmoja akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nimnusuru atakapokuwa emedhulumiwa kwa kumuondolea dhuluma, wasemaje ikiwa kadhulumu nitamsaidia vipi? Akasema: Utamzuia, na kumshika mkono na umkinge na umzuie na dhuluma; kwa kufanya hivyo ndiko kumnusuru dhidi ya Shetani wake na nafsi yake yenye kuamrisha maovu.