+ -

عَنْ وَحْشِيِّ بْنِ حَرْبٍ رَضيَ اللهُ عنه:
أَنَّهُمْ قَالُوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنَّا نَأْكُلُ وَلَا نَشْبَعُ، قَالَ: «فَلَعَلَّكُمْ تَأْكُلُونَ مُتَفَرِّقِينَ؟» قَالُوا: نَعَمْ. قَالَ: «فَاجْتَمِعُوا عَلَى طَعَامِكُمْ، وَاذْكُرُوا اسْمَ اللَّهِ عَلَيْهِ، يُبَارَكْ لَكُمْ فِيهِ».

[حسن] - [رواه أبو داود وابن ماجه وأحمد] - [سنن ابن ماجه: 3764]
المزيــد ...

Kutoka kwa Wahshiy bin Harbi radhi za Allah ziwe juu yake:
Ya kwamba wao walisema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika sisi tunakula lakini hatushibi, akasema: "Huenda nyinyi mnakula kila mtu peke yake?" Wakasema: Ndiyo. Akasema: "Basi kusanyikeni katika chakula chenu, na mkitajie jina la Mwenyezi Mungu, mtabarikiwa katika chakula hicho".

[Ni nzuri] - - [سنن ابن ماجه - 3764]

Ufafanuzi

Baadhi ya Maswahaba walimuuliza Mtume rehema na amani ziwe juu yake, wakasema: Hakika sisi tunakula lakini hatushibi.
Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema kuwaambia: Huenda nyinyi kila mtu hukaa peke yake wakati wa kula; akala kila mtu peke yake? Wakasema: Ndiyo. Akasema: Basi kusanyikeni na mle pasina kutengana, na mtaje jina la Mwenyezi Mungu wakati wa kula kwa kusema: Bismillaah, (kwa jina la Mwenyezi Mungu) mtabarikiwa ndani yake na mtashiba.

Katika Faida za Hadithi

  1. Kukusanyika kwa ajili ya chakula na kutaja jina la Mwenyezi Mungu wakati wa kula ni sababu ya kupata baraka katika chakula, na kupatikana shibe kwa kukila kwake.
  2. Utengano wote ni shari, na umoja wote ni heri.
  3. Himizo la kukusanyika na kutaja jina la Mwenyezi Mungu wakati wa chakula.
  4. Amesema Assanadi: Kwa sababu ya mkusanyika baraka huteremka katika chakula, na kwa kulitaja jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu Shetani hushindwa kukifikia chakula.
Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa الرومانية المجرية الجورجية
Kuonyesha Tarjama