+ -

عَنْ أُبَيِّ بْنِ كَعْبٍ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ:
كَانَ رَجُلٌ لَا أَعْلَمُ رَجُلًا أَبْعَدَ مِنَ الْمَسْجِدِ مِنْهُ، وَكَانَ لَا تُخْطِئُهُ صَلَاةٌ، قَالَ: فَقِيلَ لَهُ: أَوْ قُلْتُ لَهُ: لَوْ اشْتَرَيْتَ حِمَارًا تَرْكَبُهُ فِي الظَّلْمَاءِ، وَفِي الرَّمْضَاءِ، قَالَ: مَا يَسُرُّنِي أَنَّ مَنْزِلِي إِلَى جَنْبِ الْمَسْجِدِ، إِنِّي أُرِيدُ أَنْ يُكْتَبَ لِي مَمْشَايَ إِلَى الْمَسْجِدِ، وَرُجُوعِي إِذَا رَجَعْتُ إِلَى أَهْلِي، فَقَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «قَدْ جَمَعَ اللهُ لَكَ ذَلِكَ كُلَّهُ».

[صحيح] - [رواه مسلم] - [صحيح مسلم: 663]
المزيــد ...

Kutoka kwa Ubai bin Ka'ab radhi za Allah ziwe juu yake amesema:
Kulikuwa na mtu ambaye sifahamu kama kuna mtu alikuwa akiishi mbali kuliko yeye, na swala ilikuwa haimpiti, akaambiwa: Bora ungelinunua Punda ukimpanda nyakati za giza, na unapopita kwenye sehemu ya jangwa. Akasema: "Hainifurahishi nyumba yangu kuwa karibu na Msikiti, mimi ninapenda niandikiwe malipo ya kutembea kwangu, na kurudi kwangu ninaporejea kwa Watu wangu" Akasema Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake: "Hakika Mwenyezi Mungu amekukusanyia malipo yote hayo".

[Sahihi] - [Imepokelewa na Imamu Muslim] - [صحيح مسلم - 663]

Ufafanuzi

Ameeleza Ubai bin Kaab radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ya kwamba bwana mmoja katika Maanswari (watu wa Madina) alikuwa ni mtu anayeishi mbali kuliko wote kutoka ulipo Msikiti wa Mtume, na ilikuwa haimpiti swala yoyote; bali anahudhuria swala zote pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akaambiwa: Lau ungenunua punda wa kumpanda katika giza la usiku, na katika joto la Ardhi wakati wa mchana, akasema: Sipendezwi nyumba yangu kuwa karibu na msikiti, hakika mimi ninataka aniandikie Mwenyezi Mungu hatua zangu wakati wa kuja katika swala msikitini, na kurudi kwangu ninaporudi kwa watu wangu, yakafika maneno yake kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: "Hakika amekukusanyia Mwenyezi Mungu kwako yote hayo".

Katika Faida za Hadithi

  1. Pupa kubwa ya Maswahaba juu ya kheri na kuzidisha zaidi na kuchuma malipo.
  2. Amesema Nawawi: Hapa kumethibitishwa thawabu katika hatua wakati wa kurudi kutoka katika swala kama zinavyopatikana katika kwenda.
  3. Kuelezana waislamu mambo ya heri na kuusiana wema, atakayeona ndugu yake kuwa anapatwa na tabu basi amfuate na amnasihi kuziondoa tabu hizo.
  4. Nyumba kuwa mbali na msikiti si udhuru wa kuacha swala ya jamaa, maadamu mtu anasikia Adhana.
Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kiassam الرومانية المجرية الجورجية
Kuonyesha Tarjama