+ -

عن عائشةَ أمِّ المؤْمنِين رضي الله عنها قالت:
لَمْ يَكُنِ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَلَى شَيْءٍ مِنَ النَّوَافِلِ أَشَدَّ مِنْهُ تَعَاهُدًا عَلَى رَكْعَتَيِ الفَجْرِ.

[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح البخاري: 1169]
المزيــد ...

Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake, amesema:
Hakuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa na mkazo mkubwa na kudumu na jambo kama alivyokuwa katika rakaa mbili za Alfajiri.

[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح البخاري - 1169]

Ufafanuzi

Ameeleza mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake ya kwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake hakuwa na mkazo mkubwa katika swala za sunna zaidi ya jinsi alivyozikazia na kuzipupia na kuzihifadhi rakaa mbili za sunna ya kabla ya Alfajiri.

Katika Faida za Hadithi

  1. Sunna za swala ni zile zisizokuwa faradhi katika ibada, na makusudio yake hapa: Ni sunna zilizopangilia zinazofuatana na faradhi.
  2. Sunna zilizopangiliwa: Rakaa mbili kabla ya Alfajiri, na rakaa nne kabla ya Adhuhuri, na mbili baada yake, na rakaa mbili baada ya Magharibi, na rakaa mbili baada ya Ishaa.
  3. Sunna ya Alfajiri huswaliwa nyumbani na safarini, tofauti na sunna za Adhuhuri na Magharibi na Ishaa, hizo haziswaliwi isipokuwa nyumbani.
  4. Sunna hii imetikiliwa mkazo ya rakaa mbili za Alfajiri, haitakiwi kuzipuuza.
Tafsiri: Lugha ya kiingereza Lugha ya Kiurdu Kiispania Lugha ya Kiindonesia Ki ighori Kibangali Lugha ya kifaransa Kituruki Lugha ya Kirashia Lugha ya Kibosnia Kisin-hala Kihindi Kichina Kifursi Kivetenamu Kitagalogi Kikurdi Kihausa Kireno Kiassam الرومانية المجرية الجورجية
Kuonyesha Tarjama