عَنْ عَائِشَةَ رضي الله عنها قَالَتْ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:
«الْمَاهِرُ بِالْقُرْآنِ مَعَ السَّفَرَةِ الْكِرَامِ الْبَرَرَةِ، وَالَّذِي يَقْرَأُ الْقُرْآنَ وَيَتَتَعْتَعُ فِيهِ، وَهُوَ عَلَيْهِ شَاقٌّ، لَهُ أَجْرَانِ».
[صحيح] - [متفق عليه] - [صحيح مسلم: 798]
المزيــد ...
Kutoka kwa Aisha radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume rehema na amani ziwe juu yake:
"Anayesoma Qur'ani kwa uhodari huwa pamoja na msafara wa Malaika watukufu, na anayesoma Qur'ani huku anasitasita na huku kwake bado ni ngumu huyo anamalipo mara mbili".
[Sahihi] - [Wamekubaliana Bukhaariy na Muslim] - [صحيح مسلم - 798]
Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwamba anayesoma Qur'ani, akiwa na hifdhi nzuri na mfanisi, na mahiri na hodari kwa kisomo chake, basi huyu ana thawabu Akhera kiasi cha daraja yake kuwa pamoja na Malaika wema na wakarimu, na kwamba anayesoma Qur'ani na huku akipata tabu ndani yake na anasitasita katika kisomo chake; kwa sababu ya udhaifu wa hifudhi yake, lakini pamoja na hivyo bado anashikamana nayo, na kwake bado ni ngumu na nzito basi ana malipo mara mbili; malipo ya kisomo na malipo ya tabu na kusitasita kwake katika kisomo.