أتيت رسول الله صلى الله عليه وسلم وفي عنقي صليب من ذهب، فقال: «يا عدي اطرح هذا الوثن من عنقك» قال: فطرحته، وانتهيت إليه وهو يقرأ في سورة براءة، فقرأ هذه الآية: {اتخذوا أحبارهم ورهبانهم أربابا من دون الله} [التوبة: 31] قال: قلت: يا رسول الله إنا لسنا نعبدهم، فقال: «أليس يحرمون ما أحل الله فتحرمونه، ويحلون ما حرم الله فتحلونه؟» قال: قلت: بلى. قال: «فتلك عبادتهم».
[ضعيف] - [رواه الترمذي والطبري] - [تفسير الطبري: 16631]
المزيــد ...
Kutoka kwa Adiy bin Hatim-Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake-: Yakwamba yeye alimsikia Mtume rehema na Amani ziwe juu yake Akisoma aya hii: "Wamewafanya wanachuoni wao na watawa wao kuwa ni miungu kinyume na Mwenyezi Mungu na Masihi mwana wa Mariam, na hawakuamrishwa ila ni kumuabudu Mungu mmoja, hapana Mola ispokuwa yeye, ametakasika na yale wanayomshirikisha nayo" Nikasema kumwambia: Hakika sisi hatuwaabudu wao, Akasema: "Kwani hawaharamishi aliyoyahalalisha Mwenyezi Mungu nanyi mkayaharamisha? na wanahalalisha aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu nanyi mkayahalalisha? Nikasema: Ndivyo, Akasema: Basi huko ndiko kuwaabudu".
Aliposikia swahaba huyu mtukufu kisomo cha Mtume rehema na Amani zimfikie cha Aya hii ambayo ndani yake kuna habari kwa Mayahudi na wakristo: kuwa wao wamewafanya wanachuoni wao na wachamungu wao kuwa miungu, wanawawekea sheria zinazokwenda kinyume na sheria ya Mwenyezi Mungu na wakawatii juu ya hilo, ikamtatiza maana yake, kwasababu yeye alikuwa akidhania kuwa ibada inaishia katika kusujudu na mfano wake, Mtume rehema na Amani zimfikie akambainishia- kuwa katika kuwaabudu wanachuoni na watawa: ni kuwatii katika kuhalalisha haramu na kuharamisha halali, kinyume na hukumu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na Mtume wake rehema na Amani zimfikie.