عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم : «مَا يَجِدُ الشَّهيد من مَسِّ القتل إلا كما يَجِدُ أَحَدُكُمْ من مَسِّ القَرْصَةِ».
[حسن] - [رواه الترمذي وابن ماجه والنسائي والدارمي وأحمد]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Amesema: Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu -Rehema na Amani ziwe juu yake-: "Anachokipata aliyekufa shahidi katika maumivu ya kifo, ni kama maumivu anayoyapata mmoja wenu kutokana na kung'atwa na mdudu chungu".
[Ni nzuri] - [Imepokelewa na Ibnu Maajah - Imepokelewa na Imamu Tirmidhiy - Imepokelewa na An-Nasaaiy - Imepokelewa na Ahmad - Imepokelewa na Addaaramy]
Maana ya hadithi: nikuwa mtu atakapokufa shahidi katika njia ya Mwenyezi Mungu, basi hakika yale yanayompata katika mguso wa kifo, na katika riwaya ya Daaramiy (katika maumivu ya kifo) hayahisi isipokuwa ni kama anavyohisi mmoja wetu anapong'atwa na mdudu chungu, na katika riwaya ya Daaramiy "kutokana na maumivu ya kung'atwa". Na maana yake nikuwa: Shahidi hasongwi na ukali wa maumivu ya kifo, kama ilivyo hali ya watu wengine, bali ukali anaoupata na ukamsumbua wakati wa kifo chake ni kama ule tunaoupata kwasababu ya kung'atwa na mdudu chungu, na maumivu anayosababu mdudu huyo na uharaka wa kumalizika kwake, basi wala hayahisi, Na hii ni katika fadhila za Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa shahidi, kwani yeye alipoitanguliza roho yake katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kiurahisi, basi Mwenyezi Mungu akampunguzia juu yake maumivu ya kuuwawa.