عن أبي هريرة رضي الله عنه مرفوعاً: «يَدخُلُ الجّنَّة أَقْوَام أَفئِدَتُهُم مِثل أًفئِدَة الطَّير».
[صحيح] - [رواه مسلم]
المزيــد ...
Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Wataingia peponi watu vifua vyao mfano wa vifua vya ndege"
Sahihi - Imepokelewa na Imamu Muslim
Anaeleza Mtume -Rehema na Amani ziwe juu yake- kuhusu wasifu wa watu miongoni mwa watu wa peponi, nakuwa mioyo yao ni laini hupata mfadhaiko kama wanavyofadhaika ndege, na hilo ni kwasababu ya kumuogopa hao waumini Mola wao, kama ambavyo ndege mara nyingi hufadhaika na kuwa na hofu, nao pia ni watu wenye kumtegemea Mwenyezi Mungu zaidi katika kutaka shida zao kama wanavyotoka ndege asubuhi kutafuta riziki zao.